AhadiAhadi ni deni

Maswali ya kamati.

Yale yanayoulizwa kila wakati, na majibu yake bila mzunguko.

Maswali kamati zinazouliza kabla hazijaanza.

Fedha zinapita kwa Ahadi?

Hapana. Mchangiaji analipa moja kwa moja kwenye namba za kamati — M-Pesa, Mixx, Airtel Money, Halopesa au benki. Ahadi haishiki fedha yenu hata siku moja. Inarekodi tu nani ameahidi nini na nani amelipa kiasi gani.

Mchangiaji anahitaji simu janja?

Hapana. Ujumbe unakwenda kama SMS ya kawaida, inayofika kwenye kila simu hata isiyo na intaneti. Mwenye WhatsApp anaweza kuupokea huko pia kama kamati imechagua hivyo. Mchangiaji hahitaji kupakua kitu wala kufungua akaunti.

Tumeshaanza kukusanya, tuna majina kwenye daftari. Tutaandika upya?

Hapana. Pakia faili la Excel mlilonalo, au piga picha ya daftari lenu la mkono. Ahadi inaisoma na kuipanga yenyewe. Mnahakiki kabla ya kuhifadhi, na mkiona kosa mnalirekebisha.

Nani anaona namba za simu za wachangiaji?

Wanakamati pekee. Link mnayoibandika kwenye kundi la WhatsApp ni ya kusoma tu, na haionyeshi namba za simu. Mtu akitoka kwenye kamati, mnatengeneza link mpya na ya zamani inakufa.

Mtu mmoja anaweza kuwa na ahadi zaidi ya moja?

Ndiyo. Baba anaweza kuandikisha ahadi ya kila mtoto wake chini ya namba yake moja. Akistahili kumbusho, anapata ujumbe mmoja unaotaja kila mtu na salio lake — siyo ujumbe kwa kila ahadi.

Inagharimu kiasi gani?

TZS 100 kwa kila ujumbe unaotumwa. Kuandikisha wachangiaji, kurekodi malipo, ripoti na link ya kamati ni bure. Hakuna ada ya mwezi wala kiwango cha chini.

Tunaweza kuzuia vikumbusho visitumwe?

Ndiyo. Kuna chaguo la “usitume vikumbusho” kabisa, na chaguo la kuchagua vitumwe mara ngapi baada ya tarehe kupita. Mnaweza kubadilisha wakati wowote.

Taarifa za wachangiaji zinakaa kwa muda gani?

Taarifa za tukio zinafutwa miezi 12 baada ya tukio kufungwa. Kamati ndiyo mmiliki wa taarifa za wachangiaji wake; Cards Tz ni mtoa huduma. Wafanyakazi wetu wanaangalia orodha ya kamati pale tu mnapoomba msaada.

Mnafanya kazi nje ya Dar es Salaam?

Ndiyo. Ahadi inafanya kazi popote Tanzania — ni mfumo wa wavuti na ujumbe wa simu. Kadi za mwaliko pia zinatumwa kwa simu, hakuna kuchapisha wala kusafirisha.

Tunaanzaje?

Tuandikie WhatsApp 0689 786 819. Tunafungua tukio lenu, tunawaonyesha namna ya kuandikisha wachangiaji, na mnaanza. Tukio la kwanza tunalifungua pamoja nanyi.

Hujapata jibu?

Tuandikie WhatsApp 0689 786 819. Tunajibu kwa Kiswahili, na hatuuzi kitu kwa mtu asiyekihitaji.

Ahadi ni nini · Mwongozo wa kufuatilia michango · Bei

Tuanze na tukio lenu

Tuambie tukio ni lipi na lini, tunakufungulia na kukuonyesha.