AhadiAhadi ni deni

Bei ya Ahadi.

TZS 100 kwa kila ujumbe unaotumwa. Kila kitu kingine ni bure.

Unalipia ujumbe uliotumwa. Hakuna kingine.

Hakuna ada ya kujiunga, hakuna malipo ya mwezi, na hakuna kiwango cha chini. Kamati ndogo inalipa kidogo kwa sababu inatuma ujumbe mchache, siyo kwa sababu tumeipangia kifurushi.

TZS 100 kwa kila ujumbe unaotumwa

Ujumbe mmoja kwa mchangiaji mmoja. Ukichagua kutuma kwa SMS na WhatsApp pamoja, hiyo ni ujumbe miwili — mchangiaji anaupokea mara mbili, na unalipa mara mbili. Ukichagua njia moja, unalipa mara moja.

Nini hulipiwi

Kuwaandikisha wachangiaji — wangapi wowote.
Kurekodi malipo, na kuhesabu salio la kila mtu.
Ripoti ya kamati, na kuipakua kama PDF au Excel.
Link ya kusoma tu ya kundi la WhatsApp la kamati.
Kuingiza orodha mliyonayo — kutoka Excel au picha ya daftari.

Vyote hivyo ni bure. Gharama inaanza pale ujumbe unapoondoka kwenda kwa mchangiaji.

Mfano

Kamati yenye wachangiaji 50. Kila mmoja anapokea ujumbe mmoja wa uthibitisho anapoahidi, risiti anapolipa, na vikumbusho viwili kabla ya tarehe yake.

Kwa SMS pekee: ujumbe 4 × wachangiaji 50 = ujumbe 200. TZS 20,000.
Kwa SMS na WhatsApp: ujumbe 8 × wachangiaji 50 = ujumbe 400. TZS 40,000.

Mfumo unakuonyesha kadirio hili ndani ya app, likihesabiwa kutoka kwa wachangiaji wenu halisi, kabla hamjachagua. Hamuingii gizani.

Mnadhibiti wenyewe

Mnachagua njia

SMS pekee, WhatsApp pekee, au zote mbili. SMS inafika kwenye kila simu hata isiyo na intaneti. WhatsApp ni nafuu kwa mwenye intaneti. Mkichagua WhatsApp pekee, mchangiaji asiye na WhatsApp anatumiwa SMS ili asikosekane — bado ni ujumbe mmoja.

Mnachagua mara ngapi

Kuanzia “usitume kabisa” hadi kumbusho kila siku tatu. Kila chaguo linaonyesha idadi ya meseji litakayotumia kwa mwezi, kwa wachangiaji wenu halisi.

Salio linaisha, kutuma kunasimama

Kila tukio lina salio lake la meseji. Likiisha, mfumo unasimama na kuwaambia. Hakuna bili inayowakuta mwisho wa mwezi.

Kadi za mwaliko

Ahadi ni huduma ya Cards Tz. Kama tukio lenu linahitaji na kadi za wageni:

Kadi ya kawaida — kuanzia TZS 1,600 kwa kadi. Kadi ya picha yenye jina la mgeni na QR code yake.
Kadi Kamili — TZS 2,500 kwa kadi. Inaongeza ukurasa wa wavuti wenye RSVP, ramani ya ukumbi na hesabu ya siku zilizobaki.
Kuhakiki mlangoni — TZS 100 kwa kadi. Mfumo wa QR anaoutumia mwanakamati kwenye simu yake mwenyewe.

Kila kadi inakuja na kumbusho kwa mgeni siku moja kabla, ujumbe wa karibu siku ya tukio, na simu ya kuhakiki kama kadi imemfika — bila malipo ya ziada.

Tukutengenezee makadirio

Tuambie idadi ya wachangiaji na tarehe ya tukio, tunakupa hesabu halisi kabla hujaamua.