AhadiAhadi ni deni

Michango ya kamati, bila daftari.

Ahadi, malipo na vikumbusho vinavyojituma vyenyewe. Kamati inajua nani amelipa, na nani bado.

Kila kamati inajua shida hizi.

Daftari lipo kwa mtu mmoja, na siku ya kikao halipatikani.
Orodha tatu tofauti kwenye kundi la WhatsApp, zote hazilingani.
Kumkumbusha mtu ni kazi inayochosha, na wengine wanakwazika.
Mwisho wa siku, hakuna anayejua hasa kiasi kilichokusanywa.

Ahadi inafanya hivi

Unamwandikisha mchangiaji

Jina, namba ya simu, kiasi alichoahidi na tarehe ya kulipa. Anapata ujumbe wa uthibitisho papo hapo, wenye namba za kulipia.

Akilipa, unaandika

Mweka hazina anaandika kiasi na njia aliyotumia. Risiti yenye salio lililobaki inamwendea mchangiaji mara moja.

Vikumbusho vinajituma vyenyewe

Kila asubuhi, Ahadi inawatumia ujumbe wale ambao bado wana salio: siku tatu kabla, siku yenyewe, kisha kila wiki. Kamati haifanyi chochote.

Kundi linapata orodha inayojisasisha

Link moja ya kubandika kwenye kundi la WhatsApp. Inajisasisha yenyewe kila mtu anapofungua, na haionyeshi namba za simu za mtu yeyote.

Siku ya kikao, ripoti iko tayari

Mchanganuo kamili kwa PDF au Excel. Hakuna kukaa usiku kuhesabu.

Jinsi inavyoonekana

Dashibodi ya Ahadi inayoonyesha jumla ya ahadi, zilizolipwa na salio Dashibodi
Ukurasa wa kuandikisha mchangiaji mpya Rejista
Ukurasa wa vikumbusho ukionyesha ujumbe unaotumwa Vikumbusho

Fedha haipiti Ahadi

Michango inalipwa moja kwa moja kwenye namba za simu au akaunti za benki za kamati yenu. Ahadi inaandika tu kilicholipwa, kama daftari lingine lolote. Cards Tz haipokei wala haishiki mchango wa mtu yeyote.

Kamati ndiyo mwenye orodha yake. Namba za simu haziwekwi kwenye link inayoshirikishwa, na mchangiaji anaweza kuandika ACHA wakati wowote kuacha kupokea ujumbe.

Pakua mwongozo

Kurasa tatu zinazoelezea kila kitu: hatua nane, maswali yanayoulizwa, na picha za mfumo. Unaweza kuituma kwa wanakamati wenzako.

Tukio lako linakuja?

Tuambie kuhusu kamati yenu na tutakuonyesha jinsi Ahadi inavyofanya kazi, bila gharama ya kuanza.