Sera ya Faragha na Masharti ya Matumizi

Ahadi · huduma ya Cards Tz · Imeanza kutumika 1 Oktoba 2026

Kwa ufupi

Maandishi yaliyo chini ndiyo yenye nguvu kisheria. Yameandikwa kwa lugha rahisi kadri inavyowezekana.

1. Nani ni nani

Ahadi inatumiwa na kamati za matukio: harusi, sendoff, misiba, michango ya shule, na mingineyo. Watu wanaoandikwa kwenye orodha ni wachangiaji.

MhusikaWajibu
Kamati
(mtu aliyefungua tukio na wenzake)
Ndiye mmiliki wa taarifa. Anaamua nani aandikwe, kwa nini, na kwa muda gani. Anawajibika kwa wachangiaji wake.
Cards Tz
(kupitia Ahadi)
Ni mchakataji. Tunatunza taarifa na kutuma ujumbe kwa maelekezo ya kamati. Tunawajibika kwa usalama wa mfumo.
Mchangiaji Ndiye mwenye taarifa binafsi, na ana haki zilizotajwa kwenye kipengele cha 7.

Maana yake kwa vitendo: mchangiaji akiuliza kwa nini namba yake ipo kwenye mfumo, jibu linatoka kwa kamati iliyomwandika, si kwa Cards Tz.

2. Taarifa tunazokusanya

Kuhusu wachangiaji

Kuhusu wanakamati

Picha na faili

Kamati ikipakia faili la Excel au kupiga picha ya orodha, tunasoma majina na viasi vilivyomo. Picha yenyewe haihifadhiwi baada ya kusomwa.

Hatukusanyi mahali ulipo, hatufuatilii mwenendo wako mtandaoni, na hatutumii vidakuzi vya matangazo.

3. Kwa nini tunazikusanya

Msingi wa kisheria ni makubaliano kati ya kamati na mchangiaji: mtu anapoahidi mchango, anatarajia kukumbushwa. Kamati inapaswa kuhakikisha mchangiaji anajua kuwa namba yake imeandikwa.

4. Nani anaziona

5. Watoa huduma tunaowatumia

Ahadi inategemea kampuni chache za kitaalamu. Kila moja inapata kipande kidogo cha taarifa, kwa kazi maalumu tu:

Mtoa hudumaAnapata niniYupo wapi
Mtoa huduma wa SMSNamba ya simu na maandishi ya ujumbeTanzania
WhatsApp (Meta)Namba ya simu na maandishi ya ujumbeNje ya nchi
SupabaseDatabase ya orodha zoteUjerumani
NetlifyUendeshaji wa tovutiNje ya nchi
AnthropicPicha ya orodha, pale tu kamati inapotumia kameraNje ya nchi

Baadhi ya watoa huduma hawa wapo nje ya Tanzania, kwa hiyo taarifa husafiri nje ya nchi. Tunawatumia kwa sababu wanatoa ulinzi wa kiwango kinachokubalika, na hawaruhusiwi kutumia taarifa hizi kwa shughuli zao.

Hatuuzi taarifa za mtu yeyote kwa mtu wa tatu, kwa hali yoyote.

6. Muda wa kuhifadhi

7. Haki zako kama mchangiaji

Chini ya sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi ya Tanzania, una haki ya:

Njia ya haraka ni kuiambia kamati iliyokuandika, kwa sababu ndiyo yenye orodha. Ukishindwa kuipata, tuandikie info@cardstz.co.tz na tutawasiliana na kamati husika.

8. Usalama

Hakuna mfumo usio na hatari kabisa. Tukigundua uvujaji wa taarifa, tutawaarifu walioathirika na mamlaka husika bila kuchelewa.

9. Watoto

Ahadi haikusudiwi kutumiwa na watu walio chini ya miaka 18. Kamati inapaswa kutoandika mtoto kwenye orodha bila ridhaa ya mzazi au mlezi.


Masharti ya Matumizi

10. Huduma ni nini

Ahadi ni daftari la kielektroniki la ahadi na malipo, pamoja na utumaji wa ujumbe kwa wachangiaji. Inatolewa na Cards Tz.

11. Fedha

Hakuna fedha inayopita Ahadi, na Cards Tz haipokei wala haishiki mchango wa mtu yeyote. Michango inalipwa moja kwa moja kwenye namba za simu au akaunti za benki za kamati yenyewe. Ahadi inaandika tu kilicholipwa, kama daftari lingine lolote. Mgogoro wowote wa fedha ni kati ya mchangiaji na kamati.

12. Wajibu wa kamati

Kamati inayotumia Ahadi kutuma ujumbe usioombwa, au kuandika watu wasiokubali, inaweza kusitishwa bila taarifa.

13. Tunachokihakikisha na tusichokihakikisha

Tunajitahidi mfumo ufanye kazi muda wote na ujumbe ufike. Lakini ujumbe hutegemea mitandao ya simu na WhatsApp, ambayo hatuidhibiti. Hatuhakikishi kuwa kila ujumbe utafika, au utafika kwa wakati. Ahadi inaonyesha kilichotumwa na kilichofika, ili kamati ijue hali halisi.

Hatuwajibiki kwa hasara isiyo ya moja kwa moja, wala kwa michango isiyokusanywa.

14. Gharama

Gharama za kutumia Ahadi zinawekwa wazi kabla ya kuanza. Zikibadilika, kamati zinazotumia huduma zitaarifiwa kabla.

14.1 Ujumbe mmoja ni upi

Ujumbe mmoja ni ujumbe mmoja unaomfikia mchangiaji mmoja kwa njia moja. Hesabu hii haitegemei urefu wa ujumbe. Ujumbe mrefu mara nyingine hugawanywa na mtandao vipande viwili kabla kufika, na mitandao hutuchaji vipande hivyo; hata hivyo kwako huhesabiwa mmoja, kwa sababu kwenye simu ya mchangiaji ujumbe mmoja ndio unafika. Tofauti hiyo inabaki kwetu.

Vilevile:

Bei ya ujumbe mmoja kwa tukio lako inaonekana kwenye ukurasa wa Vikumbusho ndani ya mfumo, pamoja na idadi ya ujumbe uliotumwa leo, kwa siku saba, na jumla ya tukio lote. Kamati inaweza kupakua ankara ya ujumbe wakati wowote, inayoonyesha kila siku na kila aina ya ujumbe uliotumwa. Idadi kwenye ankara ndiyo hiyo iliyohesabiwa kwa kanuni hii.

15. Kusitisha

Kamati inaweza kuacha kutumia Ahadi wakati wowote na kuomba taarifa zake zifutwe. Tunaweza kusitisha akaunti inayovunja masharti haya, au inayotumia huduma kinyume na sheria.

16. Mabadiliko ya hati hii

Tunaweza kubadilisha sera au masharti haya. Mabadiliko ya msingi yataarifiwa kwa kamati zinazotumia huduma kabla hayajaanza kutumika. Tarehe juu ya ukurasa huu inaonyesha toleo la sasa.

17. Sheria inayotumika

Hati hii inaongozwa na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

18. Mawasiliano

Cards Tz
Barua pepe: info@cardstz.co.tz
Simu na WhatsApp: +255 689 786 819
Dar es Salaam, Tanzania


In English

The short version

Who is responsible for what

The committee is the data controller of its contributors' information: it decides who is entered, why, and for how long, and it answers to its own contributors. Cards Tz, through Ahadi, is the data processor: we store the information and send messages on the committee's instruction, and we are responsible for the security of the system.

What we collect

From contributors: full name, phone number, amount pledged, payments and dates, and a record of messages sent. From committee members: name, email and role. When a committee uploads a spreadsheet or photographs a list, we read the names and amounts from it; the photograph itself is not kept afterwards.

We do not collect location, we do not track browsing, and we use no advertising cookies.

Why

To keep the register, to confirm a pledge when it is made, to send a receipt when a payment is recorded, to remind those who still owe, and to produce the committee's report.

Who can see it

Only the members of that event. One committee cannot see another's. The shareable link shows a first name and an initial, the amount pledged and the amount paid, and no phone numbers and no individual due dates. Anyone holding that link can open it, so the committee should guard it, and can replace it at any time.

Service providers

An SMS provider in Tanzania, WhatsApp (Meta), Supabase for the database in Germany, Netlify for hosting, and Anthropic for reading a photographed list when a committee uses the camera. Some of these are outside Tanzania, so data crosses borders. None of them may use the data for their own purposes. We never sell personal data.

How long we keep it

While the event is open, then 12 months after it is closed, then deleted. A committee may ask for deletion sooner, and we act within 30 days.

Your rights

Under Tanzanian personal data protection law you may ask what is held about you, correct it, have it deleted, object to its use, and stop receiving messages. The fastest route is the committee that entered you, since the list is theirs. If you cannot reach them, write to info@cardstz.co.tz.

Security

All traffic is encrypted. Each committee sees only its own event, enforced in the database itself rather than on screen. Provider keys stay on the server and never reach the app. The list link carries a long unguessable code and can be revoked. No system is without risk; if data is exposed we will tell those affected and the authorities without delay.

Terms of use

No money passes through Ahadi, and Cards Tz never receives or holds anybody's contribution. Contributions are paid directly to the committee's own accounts; Ahadi records what was paid, as any ledger does. Any dispute about money is between the contributor and the committee.

The committee undertakes to enter only the numbers of people who agreed to be entered and who know they will receive messages, to keep the information accurate, to use the list only for that event, to guard the shareable link, and not to share its account password. An account used to send unsolicited messages may be suspended without notice.

We work to keep the service running and messages flowing, but delivery depends on mobile networks and WhatsApp, which we do not control. We cannot guarantee that every message arrives, or arrives on time. We are not liable for indirect loss, nor for contributions that go uncollected.

What counts as one message: one message is one message delivered to one contributor on one channel, whatever its length. A long message is sometimes split into two parts by the network before it arrives, and the networks charge us for both parts โ€” but it counts as one to you, because one message is what reaches the contributor's phone. One number shared by two people receives one message naming both and counts as one. A committee that chose both channels pays for two messages per contributor, because two are sent, and the app says so before the choice is made. A message that does not arrive is not charged, and its credit is returned at once. The price per message, the counts for today, for the last seven days and for the whole event, and a downloadable invoice, are all in the app under Reminders.

A committee may stop using Ahadi at any time and ask for its data to be deleted. We may suspend an account that breaks these terms or uses the service unlawfully. We may change this document; material changes will be notified before they take effect. This document is governed by the laws of the United Republic of Tanzania.

Kwa maswali yoyote kuhusu hati hii: info@cardstz.co.tz